Ezekiel 30:6-11

6 a“ ‘Hili ndilo Bwana asemalo: “ ‘Wale walioungana na Misri wataanguka
na kiburi cha nguvu zake kitashindwa.
Kutoka Migdoli hadi Aswani,
watauawa ndani yake kwa upanga,
asema Bwana Mwenyezi.


7 b“ ‘Hizo nchi zitakua ukiwa
miongoni mwa nchi zilizo ukiwa,
nayo miji yao itakuwa magofu
miongoni mwa miji iliyo magofu.

8 cNdipo watakapojua kwamba mimi ndimi Bwana,
nitakapoiwasha Misri moto
na wote wamsaidiao watapondwa.

9 d e“ ‘Siku hiyo wajumbe watatoka kwangu kwa merikebu, ili kuwatia hofu Ethiopia, wakiwa katika hali yao ya kuridhika. Maumivu makali yatawapata siku ya maangamizi ya Misri, kwa kuwa hakika itakuja.

10 f“ ‘Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: “ ‘Nitakomesha makundi ya wajeuri ya Misri
kwa mkono wa Nebukadneza mfalme wa Babeli.

11 gYeye na jeshi lake, taifa lililo katili kuliko mataifa yote,
litaletwa ili kuangamiza nchi.
Watafuta panga zao dhidi ya Misri
na kuijaza nchi kwa waliouawa.
Copyright information for SwhKC